Speakers Conference: Shigongo, Harris Kapiga Wawanoa Vijana – Video

HATIMAYE ule mkutano wa kihistoria na wa aina yake uliopewa jina la Speakers Conference umefanyika Jumamosi iliyopita katika Ukumbi wa Mikutano wa Kilimanjaro uliopo Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na mamia ya watu kutoka kada mbalimbali.

 

Speakers Conference (Season 2) ulianza majira ya saa 2:30 asubuhi huku watoa mada mbalimbali wakizungumza na kutoa mbinu mbalimbali hasa kwa vijana ili kujitegemea na kuanzisha biashara za ndoto zao ili kuyafikia mafanikio yao.

Mkutano huo uliwakutanisha wahamasishaji wa masuala ya maendeleo na mafanikio, washauri, walimu wa ujasiriamali, watangazaji na waandaaji wa vipindi vya redio na televisheni, wafanyabiashara, wakufunzi, wajasiriamali na wahamasishaji chipukizi na watu wengine wa kawaida.

Lengo kubwa la mkutano huo ulioandaliwa na Taasisi ya Road to Success ni kuwajengea uwezo vijana wa kuzitambua fursa kutoka katika maeneo wanayoishi na kuzifanya kuwa biashara ili ziwaingizie vipato na kujikwamua kimaisha, hivyo kuondokana na umaskini ama utegemezi wa ajira kutoka serikalini ama mashirika mbalimbali.

Miongoni mwa watu waliohudhuria katika mkutano huo, ni Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Global Group, Eric Shigongo ambaye pia ni mhamasishaji na mwalimu wa ujasiriamali, Sophia Mbeyela, Chris Mauki, Anthony Luvanda, Harris Kapiga na wengine kibao.

 

Mkutano huo ulidhaminiwa na Global Publishers Ltd, EFM, MC Rhevan Online, Happiness Massage Clinic, FAPI, FABI Events, Megafin, Singo na SUS.

 


Loading...

Toa comment