Spika Mstaafu Ataka Tafiti Kwanini Wavulana Wanashuka Kitaaluma
SPIKA mstaafu Anne Makinda ambaye pia ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kairuki amependekeza zifanyike tafiti kujua sababu za watoto wengi wa kiume kuachwa nyuma kitaaluma na wenzao wa kike.
Aliyasema hayo jana wakati wa kongamano la sita kitaaluma lililoandaliwa na chuo hicho kujadili namna sekta ya afya inaavyoweza kufanya mabadiliko kwa huduma hizokutolewa kidijitali.
Alisema kwa siku za karibuni watoto wa kike wameonekana kuongoza kitaaaluma na kuwaacha mbali wenzao wa kiume jambo ambalo alisema jamii haipaswi kulifumbia macho na kuliona kama la kawaida.
“Hili si jambo la kawaida kabisa na tusilichukulie kirahisi lazima tutafute sababu za kwanini hawa watoto wanaanguka kitaalu…
Picha mbalimbali za kongamano la sita la kitaaluma.la Chuo Kikuu Kairuki leo jijini Dar es Salaam