The House of Favourite Newspapers

Spika Ndugai Asema Atakwenda Kwa Tundu Lissu Baada ya Krismasi

Ndugai akijadili jambo na issu.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai (Mb.) ameusema kuwa atakwenda nchini Kenya kumuona Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (CHADEMA) ambaye anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Nairobi nchini Kenya kufuatia kushambuliwa kwa risasi, Septemba 7, 2017.

 

Ndugai amesema hayo leo Desemba 15, 2017 alipokuwa akizungumza na wanahabari nyumbani kwake Mjini Dodoma kueleza kuwa watakwenda kumuona Tundu Lissu kwani ni mbunge wao na wao wanampenda sana. Ameeleza kuwa kipindi cha nyuma alishindwa kwenda Kenya kwa kuwa nchi hiyo ilikuwa kwenye uchaguzi na haikuwa na utulivu wa kisiasa, laakini kwa kuwa sasa imetulia anatarajia kwenda baada ya Sikukuu ya Christmas ili kumjulia hali.
“Mimi kama Spika siwezi kwenda na kutoka Kenya ninavyotaka, bali napokwenda kule lazima kuwe na taarifa rasmi za kiserikali na kibunge na ninapokelewa hivyo na ninapopelekwa huko hospitali au wapi napelekwa kwa utaratibu huo ndiyo utaratibu wa nchi kwa nchi.

 

“Haiwezekani wao wana mechi kama zile (Uchaguzi) halafu spika nazunguka zunguka Nairobi wanaweza kusema ajenda aliyokuja nayo huyu siyo hii, katika pande hizi mbili Watanzania wamemtuma huyu ana ajenda nyingine kwa hiyo unapokuwa kiongozi lazima ujiongeze,” alisema Ndugai.
Ndugai aliendelea kuelez; “Haukuwa wakati mzuri kwenda Nairobi, ila kwa kuwa haya mambo yamepita na serikali imekaa sawa sawa, basi tusubiri Christmas ipite baada ya hapo mtamuona Spika muda si mrefu akienda kumuona Mbunge wake Nairobi au mahali pengine popote pale. Yule ni Mbunge wetu na tunampenda sana na tusingependa asikitike kwa lolote lile,” alimalizia Ndugai.

 

VIDEO:

MASKINI… Miaka 20 ya Binti JUDITH Kitandani, Alizaliwa na Sura ya Ajabu!

 

Comments are closed.