The House of Favourite Newspapers

Spika Ndugai Azungumzia Ofisi ya CAG: “Hakuna Anayebaki”

SPIKA wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai, ameeleza amepokea taarifa ya kufanyiwa ukaguzi kwa ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Mussa Assad, ambao umefanya na kampuni binafsi na yeye kuikabidhi kwenye Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) na kusema baada ya uchambuzi ataisoma taarifa hiyo bungeni.

 

Ametoa kauli hiyo bungeni jijini Dodoma wakati wa mwendelezo wa vikao vya Bunge la 11 jijini humo, ambapo amesema  kuwa katika suala la ukaguzi hakuna taasisi inayolikwepa.

 

“Ningependa kuwajulisha juu ya taarifa ya ukaguzi wa ofisi ya CAG kwa mwaka wa fedha unaoshia Juni, 2018.  Hesabu za CAG zinapaswa kukaguliwa walau mara moja kwa mwaka, na Kamati ya PAC ndiyo ina jukumu la kukagua ofisi hiyo.  Kazi imeshafanyika na imetuletea taarifa ya hesabu zilizokaguliwa za ofisi hiyo.

 

“Taarifa ya kukaguliwa ofisi ya CAG, nimeshaipitia, lakini kiutaratibu nimeshaipeleka PAC na wakishamaliza uchambuzi watawasilisha kwangu, niwataarifu kwenye masuala ya ukaguzi hakuna anayebaki, kila watu wanawakagua wenzao,” alisema.

 

Ndugai na Profesa Assad wamekuwa kwenye mgogoro wa muda mrefu kufuatia kauli aliyoitia (Assad) akiwa nchi za nje kwamba bunge hilo ni dhaifu katika kudhibiti na kusimamia mahesabu ya serikali.

Comments are closed.