The House of Favourite Newspapers

SPORT XTRA LAZIDI KUJIIMARISHA KWA WASOMAJI

Ofisa Mauzo, Charles Mponza (kulia) akiwaelekeza jambo wasomaji wa Spoti Xtra wa Mbagala Charambe, Dar.

KIKOSI cha mauzo cha kampuni ya Global Publishers Ltd (GPL) watoaji wa magazeti ya Uwazi, Ijumaa, Ijumaa Wikienda, Risasi, Championi na Spoti Xtra, leo Jumapili kimeingia tena mitaani na kuwafikishia wasomaji gazeti maarufu nchini la michezo na burudani,  Spoti Xtra,  ambapo walionekana kuligombea baada ya kuanza kulizoea kwa habari zake motomoto, zikiwemo makala za burudani, michezo, hadithi za kusisimua na katuni.

Wasomaji hao wameomba magazeti hayo yasambazwe kwa wingi sehemu mbalimbali ili waweze kuyapata  kwa urahisi. Leo kikosi hicho kilitembelea maeneo ya Mbagala-Zakhem, Charambe, Kizuiani Vikindu na kwengine.

Matukio katika picha:

Mama-lishe akijipatia gazeti pendwa la michezo la Spot Xtra.

Said Ahmed wa Mbagala (kushoto) akikabidhiwa jezi na Ofisa Mauzo wa GPL, Bilal Songoro (kulia).

 

 

Wasomaji wa Mbagala-Zakhem na Vikindu walivyolichangamkia Spoti Xtra leo.

PICHA ZOTE NA RICHARD BUKOS

 

Comments are closed.