The House of Favourite Newspapers

SportPesa Yaitunuku Global Publishers Tuzo

0
Kutoka kulia ni Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho, Kaimu Mhariri Kiongozi wa Gazeti ya Championi, Elius Kambili na Mhariri wa Championi Jumatano, Philip Nkini wakimkaribisha Ofisa Uhusiano wa SportPesa, Sabrina Msuya alipowasili kwenye Ofisi za Global Publishers zilizopo Mwenge Bamaga, Dar.

KAMPUNI ya kubashiri matokeo ya SportPesa imeikabidhi Kampuni ya Global Publishers kupitia Gazeti la Championi tuzo kutokana na ushirikiano mzuri ambao wamekuwa nao.

Sabrina Msuya akionyesha tuzo hiyo.

SportPesa imeikabidhi Global Publishers tuzo hiyo leo ikishukuru kutokana na ushirikiano mzuri ambao kupitia Gazeti la Championi ilionyesha kwa kampuni hiyo mara baada ya timu ya Everton kutua hapa nchini mwezi Julai.

Sabrina Msuya akikabidhi tuzo hiyo kwa Kaimu Mhariri Kiongozi wa Gazeti ya Championi, Elius Kambili.

“Tunashukuru kwa ushirikiano wenu kuanzia tulipoanza kufanya kazi nanyi, lakini pia mlituonyesha ushirikiano mzuri sana wakati timu ya Everton ilipotua hapa nchini kucheza na Gor Mahia,” alisema Ofisa Uhusiano wa Sportpesa Sabrina Msuya.

Kutoka kushoto ni wahariri wa Championi, Philip Nkini, John Joseph na Elius Kambili wakiwa na tuzo hiyo baada ya kukabidhiwa.

 

Tuzo yenyewe.

 

Wahariri wa Championi wakijadili jambo na viongozi wa Sportpesa kuhusu Gazeti la Championi Jumatano lililopo mtaani leo.

 

Kutoka kushoto ni wahariri, John Joseph, Philip Nkini, Elius Kambili wakiwa na Sabrina katika picha ya pamoja.

PICHA NA ABEID LIJEY | GPL

Leave A Reply