Sportpesa Yaipa Mwaka Mwingine Namungo Fc

KAMPUNI ya mchezo ya kubashiri matokeo ya mpira, nchini ya Sportpesa, kupitia kwa mkurugenzi wa utawala na udhibiti wa Sportpesa, Tarimba Abbas, leo Februari 17, wamesaini mkataba mpya wa mwaka mmoja ukiachilia mbali ule wa awali na amekabidhi kiasi cha shilingi milioni 120, ili kuiendelea kuidhamini Klabu ya Namungo FC,

Mkataba huo umeendana sambamba na kitita cha Shilingi milioni 120, ambazo zimekabidhiwa kwa Mwenyekiti wa klabu hiyo Hassan Zidadu Kungu, aliyekuwa sambamba na straika wao raia wa Ghana Steven Sey.

