SportPesa Yamwaga Vifaa vya michezo Ruangwa


KAMPUNI ya michezo ya kubashiri ya SportPesa Tanzania, imeunga mkono juhudi za Waziri Mkuu na Mbunge wa Ruangwa Muheshimiwa Kassim Majaliwa za kuendeleza michezo kwenye wilaya ya Ruangwa baada ya jana kumwaga vifaa vya michezo

Vifaa hivyo walivyovitoa SportPesa ni kutoka timu mbalimbali ambazo inazidhamini Ulaya kwa ajili ya kuisaidia michezo Afrika kupitia kamoeni ya SportPesa inayojulikana kama Kits For Afrika.


SportPesa ambayo inaidhamini na timu ya Namungo FC ya Ruangwa ilipata nafasi ya kutembelea mkoani hapa na kuzungumza na baadhi ya viongozi wa timu mbalimbali za hapa hiyo yote katika kuunga mkono juhudi za Majaliwa katika kuhakikisha soka linakuwa.

Akizungumza na timu hizo, Tarimba alisema kuwa katika kutambua umuhimu wa michezo, SportPesa imeona ni vema ikatoa vifaa vya michezo ikiwemo mipira na lengo ni kuona vijana wanapata mafanikio kama ilivyokuwa kwa Mbwana Samatta anayeichezea Aston Villa ya Uingereza.

Tarimba alisema wamevutiwa na mwenenendo wa Namungo inayoshika nafasi ya nne katika msimamo wa Ligi Kuu Bara na kushawishika kumwaga vifaa Ruangwa.

Aliongeza kuwa, huo ni mwanzo kwa timu nane za Ruangwa walizowapatia zawadi za vifaa vya michezo huku wakipanga kuzipa timu nyingine hapo baadaye zikiwemo jezi mpya.

“SportPesa kama kampuni ya ubashiri hapa nchini, imeona vema kuunga mkono juhudi za Waziri Mkuu na Mbuge wa Ruangwa, Majaliwa katika kuendeleza michezo katika wilaya yake.

“Kwa kuanza, tumeanza na timu nane kubwa za wilayani hapa Ruangwa na baadaye tutaona tena vifaa vingine vya michezo zikiwemo jezi kama ilivyokuwa Namungo inayofanya vizuri katika ligi.

“SportPesa imekuwa sehemu ya kuunga michezo hapa nchini na ikumbukwe kuwa SportPesa iliwahi kuzileta klabu kubwa za kutoka Ulaya ikiwemo Everton inayoshiriki Ligi Kuu ya Uingereza na Sevilla inayocheza La Liga ya huko Hispania,” alisema Tarimba.

Toa comment