The House of Favourite Newspapers
gunners X

SportPesa Yazawadia Yanga Tsh Milioni 262.5 kwa Mataji Matano!

Kampuni ya kubashiri michezo ya SportPesa, ambayo pia ni mdhamini mkuu wa Klabu ya Young Africans SC, imeikabidhi klabu hiyo hundi ya shilingi milioni 262.5 kama zawadi ya bonus kufuatia mafanikio makubwa ya kutwaa mataji matano katika msimu wa 2024/2025.

Akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa SportPesa Tanzania, Abbas Tarimba, alisema:

“Kwenye mkataba wetu tulikubaliana kuwa na zawadi ya gawio kama sehemu ya matokeo haya ya kuwa na msimu bora na wenye mafanikio. Leo tunakabidhi hundi ya Tsh 262.5 milioni kwa Young Africans SC kwa kufikia mafanikio haya. Kampuni ya SportPesa kwa kipindi cha miaka saba hatujawahi kukosa kutimiza sharti letu la kimkataba.”

Bonus hiyo ni sehemu ya makubaliano ya kimkataba kati ya SportPesa na Yanga SC, ambapo mafanikio ya klabu katika mashindano mbalimbali huzingatiwa kama kipimo cha motisha na kutambua mchango wa klabu kwa mdhamini.

Young Africans SC imekuwa na msimu wa kihistoria baada ya kunyakua mataji matano, ikiwemo ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Kombe la FA, Ngao ya Jamii, pamoja na mafanikio katika ngazi ya kimataifa na kitaifa.

Comments are closed.