The House of Favourite Newspapers

Sportpesa Yazindua Shinda Na Sportpesa, Watu 100 Kushinda Bajaj

0
Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji wa SportPesa, Bwana Tarimba Abbas akiongea na wanahabari.

Kampuni ya michezo ya kubashiri nchini ya SportPesa Oktoba 25 imezindua rasmi kampeni ya SHINDA NA SPORTPESA itakayodumu kwa siku 100 ambapo mshindi mmoja ataweza kujishindia TVS KING mpya kila siku.

Kwenye promosheni hiyo, sambamba na washindi kuondoka na TVS KING mpya kila siku, lakini pia kutakuwa na zawadi nyingine zinazoshindaniwa ambazo ni pamoja na tiketi tatu kwenda nchini Uingereza kutazama mechi ya EPL, tiketi moja ikitolewa kila mwezi sambamba na jezi orijino zitakazotolewa kila wiki.

Akizungumza kwenye uzinduzi wa promosheni hiyo uliofanyika kwenye Uwanja wa Bakhresa, Manzese jijini Dar es Salaam asubuhi ya leo, Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji wa SportPesa, Bwana Tarimba Abbas amesema kuwa promosheni hiyo ina lengo la kubadili maisha ya watanzania kiuchumi.

Tarimba Abbas akizindua namba ya kutuma 15888

“Sisi kama kampuni tumeona umuhimu wa kuja na promosheni hii ili kuweza kuwainua wateja wetu kiuchumi na kuwaongezea fursa ya kujipatia kipato zaidi. Kama ulikuwa na TVS KING moja basi tunakuongezea ya pili ili uongeze kipato zaidi na kama ulikuwa huna kabisa basi tunakupa hii moja ili uanze leo.

Jinsi ya kushiriki
Baada ya kusema hayo, Bwana Tarimba alitoa ufafanuzi jinsi ya kushiriki kwenye promosheni hiyo ili kuweza kushinda TVS KING mpya kama ifuatavyo;

“Kwanza ni lazima tukumbuke kuwa kila siku kutakuwa na mshindi hivyo watakaopata fursa ya kushinda ni wale watakaokuwa wakicheza na SportPesa tu.

 

“Kama bado hujawahi kucheza na SportPesa basi hakikisha unajisajili kwa kutuma neno GAME kwenda 15888 na baada ya hapo utatakiwa kuweka pesa kwenye akaunti yako ya SportPesa kwa namba ya biashara 150888 kisha piga *150*87# au tembelea www.sportpesa.co.tz KUWEKA UTABIRI wako mara nyingi zaidi ili uweze kuingia kwenye droo.

“Hakuna uchawi mwingine wa kushinda TVS KING mpya zaidi ya kuweka ubashiri wako na SportPesa na hii ni fursa pekee ya kujiajiri na kubadili maisha yako kwasababu sote tumekuwa mashahidi jinsi ambavyo vijana wengi leo hii wamejiajiri au kuajiriwa kupitia TVS KING.

Hii itakuwa ni promosheni ya pili kutangazwa na Kampuni ya SportPesa ambayo ni mdhamini mkuu wa klabu za Simba, Yanga na Singida United baada ya ile ya kwanza ya Zali la Mwanaspoti itakayodumu kwa wiki nane ambayo kila wiki mshindi mmoja anajishindia tiketi ya kwenda nchini Uingereza kutazama mechi ya EPL huku mshindi wa kwanza akiwa ameshapatikana.

Leave A Reply