The House of Favourite Newspapers

SPOTI HINTS: OKWI, JUUKO OUT! AFRICAN LYON VS SIMBA – VIDEO

LIGI Kuu Tanzania Bara inaendelea tena leo kwa michezo mbalimbali kupigwa katika viwanja Tofauti ikiwemo Mechi kati yaAfrican Lyon dhidi ya Simba katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha huku Kocha Mkuu Patrick Aussems akithibitisha kuwakosa wachezaji wake Emmanuel Okwi na Juuko Murshid.

Lakini pia gumzo ambalo lilikuwa likiendelea katika mitandao ya kijamii ikimuhusu Beki Mkongwe Kelvin Yondani kutompa mkono Nahodha wake Ibrahim Ajibu leo wanayanga wameamua kuonyesha video ambayo inawaonyesha wako sawa huku wakikimbizana katika kambi yao waliyoweka jijini Mwanza wakijiandaa na mchezo wao dhidi ya Mbao FC.

Comments are closed.