The House of Favourite Newspapers

SPOTI XTRA LAZIDI KUWASHIKA MTAANI – VIDEO

Wafanyakazi wa Global Publishers wakiongozwa na Meneja wao Mkuu, Abdallah Mrisho (kushoto) wakiwa maeneo ya Ubungo wakinadi Gazeti la Spoti Xtra.

 

TIMU-kazi ya wachapishaji wa gazeti la SPOTI XTRA, mapema leo imezama tena mitaa mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam kwa ajili ya kulinadi gazeti hilo ambalo lilikuwa likitoka mara moja kwa wiki na sasa linatoka mara mbili kwa maana ya siku ya Alhamisi na Jumapili kwa bei ya shilingi 500.

Mrisho akimuuzia Spoti Xtra mwendesha bodaboda.

Gazeti hili linalochapishwa na Kampuni ya Global Publishers Ltd, limeendelea kuwashika vilivyo wasomaji wake mbalimbali kiasi cha kuutaka uongozi uzidishe zaidi usambazaji wake ili liwafikie watu wengi, tofauti na lilivyo sasa ambapo limekuwa likinunuliwa na kuisha kabisa huku likiwaacha baadhi yao na kiu ya kulisoma.

Mrisho akilinadi Spoti Xtra kwa waendesha bodaboda maeneo ya Ubungo.

Akizungumzia ujio huo wa gazeti hilo la Spoti Xtra kila Alhamisi, Mrisho amesema lengo kubwa ni kumaliza kiu ya wapenzi wa habari za michezo na ndiyo sababu kubwa ya kuliingiza mtaani Alhamisi na Jumapili.

Spoti Xtra limesheheni takwimu za soka na michezo mbalimbali inayopendwa duniani, uchambuzi makini wa mechi na masuala ya michezo bila kusahau ratiba na matokeo ya ligi zote kubwa duniani.

Venda aking’arishwa na Spoti Xtra.

Aidha, Spoti Xtra limesheheni makala za kuvutia za michezo, stori za burudani na mastaa wa ndani na nje ya nchi.

Na kofia ya Spoti Xtra juu.

 

Unaambiwa kwamba, Spoti Xtra linakupa uhondo zaidi kwa #Jero, pia linakupa fursa ya kushinda zawadi kibao zikiwemo jezi orijino za timu za Ulaya uzipendazo.

Picha zote hizi zinaonyesha baadhi ya wafanyakazi wa gazeti la SPOTI XTRA wakiwa katika mitaa ya Makumbusho, Morocco, Magomeni na Karume,  Ilala tayari kulinadi gazeti hilo ambalo wasomaji wake wamelipenda na kuendelea kuahidi kulisoma kila siku ya Alhamisi na Jumapili linapoingia mitaani.

Mfanyakazi wa Global Publishers, Samwel Shigongo akinadi Spoti Xtra na Amani.

 

Mwandishi wa Spoti Xtra, Lucy Mgina akinadi Spoti Xtra.

 

 

Mhariri Kiongozi wa Global Publishers, Amrani Kaima akiwa na mwandishi wake, Shamuma wakilinadi Spoti Xtra.

 

 

PICHA NA DENIS MTIMA | GPL

Comments are closed.