The House of Favourite Newspapers

Spoti Xtra Lilivyochangamkiwa Kibamba Mpaka Mloganzila

Muusomaji wa Kibamba Shule ilibidi kila mmoja apate gazeti lake ili kupata uhondo wa gazeti hilo kwa wakati muafaka.
Mfanyabiashara wa Soko Dogo la Kibamba Msikitini akijipumzisha kwa kusoma Spoti Xtra.
Afisa Masoko wa Global Publishers, Keffa Massaga akiomuonesha msomaji habari ambazo si rahisi kuzipata kwenye magazeti mengine.
Wakazi wa Kibamba Msikitini wakiangalia kiumakini habari habari zilizoandikwa kwenye gazeti hili
Mkazi wa Kibamba Kibwegele akipokea zawadi ya sabuni kutoka kwa muuzaji wa magazeti ya Spoti Xtra, Ashura Hassan.

GAZETI bora la michezo linalokuja kasi la Spoti Xtra ambalo linatoka kila jumapili leo limezidi kukimbiza mitaani katika viunga mbalimbali vya Dar na nchi nzima kwa ujumla.

Sambamba na wauzaji wanaosambaza gazeti hilo nchini nzima kikosi cha promotion cha gazeti hili nacho kama kawaida kiliingia mitaani ambapo kilianza kulitangaza Spoti Xtra maeneo ya Makao Makuu ya Ofisi za Global Publishers, Sinza Mori Dar na kuelekea sehemu mbalimbali.

Kikosi kazi hicho baada ya kutoka maeneo ya ofisini hapo kilielekea maeneo ya Kimara Mbezi, Kibamba Msikitini, Kibamba Shule mpaka Mlonganzila.

Maeneo yote hayo kikosi hicho kilikuwa kikilinadi gazeti hilo ambapo wasomaji walibahatika kulinunua sambamba na gazeti hilo walipatiwa zawadi mbalimbali kutoka kwa maofisa waliokuwa wakilinadi gazeti hilo.

AIDHA, kuanzia toleo la leo, msomaji wa Spoti Xtra atakuwa ana nafasi ya kujishindia Headphones za kisasa za Beats By Dr. Dre ambazo ni orijino. Ili kujishindia Headphones hizo, maalum kwa kusikilizia muziki, nunua nakala ya gazeti hilo na kisha fuata maelekezo rahisi ambayo yanapatikana ukurasa wa pili.

(HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS)

Comments are closed.