The House of Favourite Newspapers

Spoti Xtra Lilivyokimbiza Viunga vya Jiji la Dar leo (Picha + Video)

Wasomaji wakiendelea kupata uhondo wa Gazeti la Spoti Xtra maeneo ya Mbagala jijini Dar leo.
…Wasomaji wengine walikutwa wakisoma Gazeti la Spoti Xtra.
Wakazi wa Kitunda jijini Dar wakiangalia kiumakini  habari zilizoandikwa kwenye gazeti hilo.
Mkazi wa Mbagala akipokea zawadi ya sabuni kutoka kwa muuzaji wa magazeti ya Spoti Xtra, Ashura Hassan.

GAZETI bora la michezo linalokuja kasi la Spoti Xtra ambalo linatoka kila jumapili leo limezidi kukimbiza mitaani katika viunga mbalimbali vya Dar na nchi nzima kwa ujumla.

Wauzaji wanaosambaza gazeti hilo nchini nzima kikosi cha promotion cha gazeti hili nacho kama kawaida kiliingia mitaani ambapo kilianza kulitangaza Spoti Xtra maeneo ya Mbagala jijini Dar na kuelekea sehemu mbalimbali.

Maeneo yote hayo kikosi hicho kilikuwa kikilinadi gazeti hilo ambapo wasomaji walibahatika kulinunua sambamba na gazeti hilo walipatiwa zawadi mbalimbali kutoka kwa maofisa waliokuwa wakilinadi gazeti hilo.

Msomaji wa Spoti Xtra atakuwa ana nafasi ya kujishindia Headphones za kisasa za Beats By Dr. Dre ambazo ni orijino na jezi mbalimbali. Ili kujishindia Headphones na jezi hizo, maalum kwa kusikilizia muziki, nunua nakala ya gazeti hilo na kisha fuata maelekezo rahisi ambayo yanapatikana ukurasa wa pili.

Comments are closed.