SPOTI XTRA SASA GUMZO KILA KONA
KIKOSI cha mauzo cha magazeti ya Global Publishers, leo kimeingia tena mtaani kulinadi gazeti jipya na bora la michezo la Spoti Xtra ambalo liliendelea kuwa gumzo na kugombewa na wasomaji kila kona. Wiki hii kikosi hicho kilitembelea maeneo ya Boko, Bunju, Wazo Hill na kwingineko.
Wasomaji pamoja na kujisomea uhondo wa matukio yaliyomo, zikiwemo takwimu mbalimbali za michezo na katuni, kuna sehemu yenye kuponi ambayo wasomaji walijaza kwa ajili ya kujishindia zawadi mbalimbali zikiwemo kofia na jezi za timu mbalimbali ulimwenguni.
Matukio katika Picha:
Wafanyakazi wa Lulu Executive Beauty Salon ya Bunju B, jijini Dar wakifurahia gazeti la Spoti Xtra baada ya kutembelewa na kikosi cha usambazaji ofisini kwao leo Alhamisi.
Wasomaji wa Boko CCM, wakielekezana jambo ndani ya Spoti Xtra.
Wasomaji wa Wazo Hill, wakijadili jambo la burudani ndani ya Spoti Xtra baada ya kutembelewa na kikosi cha usambazaji cha magazeti ya Global.
Wasomaji wa Boko Basihaya wakipata uhondo wa Spoti Xtra.
Washikaji wa kijiwe cha Bodaboda cha Boko Chama wakichangamkia Spoti Xtra.
Madereva wa Bunju Shule wakiburudika na Spoti Xtra.
PICHA ZOTE NA RICHARD BUKOS
Comments are closed.