The House of Favourite Newspapers

Spoti Xtra Yamwaga Jezi kwa Wasomaji Wake

Mhariri Msaidizi wa Gazeti la Spoti Xtra, Samson Mfalila (kulia) akimkabidhi Alfred Peter zawadi ya jezi kwa niaba ya mshindi Fadhili Hassan aliyeko Tanga.

 

Washindi wawili wa shindano la gazeti la Spoti Xtra la zawadi za Headphone za Beats by Dre Original kutoka Marekani na jezi za timu za Ligi Kuu England wamekabidhiwa zawadi zao leo Jumatatu kwenye Ofisi za Global Publishers, zilizopo Sinza Mori jijini Dar es Salaam.

 

 

Mfalila (kulia) akikabidhi jezi Mshindi, Gaston Shayo.

 

Mkazi wa Manzese jijini Dar es Salaam, Gaston Shayo na Fadhili Hassan wa Handeni, Tanga ndiyo waliibuka washindi wa zawadi za jezi, ambapo walipewa jezi za timu ya Chelsea, ambayo wanaishabikia kwenye Ligi Kuu ya England.

 

Shayo na Fadhili, ambaye aliwakilishwa na jamaa yake Wilfred Peter, waliishukuru kwa zawadi hiyo na kuhimiza watu kusoma gazeti bora la Spoti Xtra linalotoka kila Jumapili kwa kuwa lina habari za kina za michezo na zenye takwimu na pia watajipatia nafasi ya kujishindia zawadi.

Comments are closed.