The House of Favourite Newspapers
gunners X

Staa wa kikapu afichua siri

Image result for Baraka Sadick

BAADA ya kutangazwa kuwa mfungaji bora wa michuano ya Majeshi kwa Jumuiya ya nchi za Afrika Mashariki, hivi karibuni, mchezaji nyota wa kikapu anayeitumikia timu ya JKT ya jijini Dar, Baraka Sadick amefichua siriinayomfanya atakate katika kila mashindano.

 

Akizungumza na Championi Jumatatu, Baraka alisema kuwa nidhamu, kujituma ndani na nje ya uwanja, mazoezi ya mara kwa mara, utii na usikivu kwa kocha wake ndiyo silaha anazotumia kuvuna matokeo chanya katika mashindano tofauti dhidi ya wapinzani.Mbali na hilo.

 

Baraka aliongezea kuwa umoja uliopo baina yake na wachezahji wa timu ya JKT lakini pia nidhamu ya hali ya juu inayopatikana ndani ya kikosi hicho ndiyo inampa nguvu ya kujituma uwanjani katika kuhakikisha anaiwakilisha vema klabu yake na Tanzania kwa jumla.

Related image

.“Mpaka sasa nina historia ya kushinda taji la ufungaji bora mara nane kupitia mashindano tofauti ya ndani na nje ya Tanzania yakiwemo haya ya majeshi ya mwaka huu ambapo kwa upande wa matokeo ya jumla hatujabeba kombe kutokana na ushindani uliokuwepo.

 

“Siri kubwa ya jina langu kuendelea kutakata katika kila mashindano ni kujituma, nidhamu, ushirikiano lakini pia usikivu wa wachezaji wenzangu na kocha katika kupeana ushauri wa hapa na pale kusaka matokeo chanya uwanjani,” alifafanua.

 

Mbali na Baraka kuibuka mfungaji bora wa mashindano ya majeshi yaliyofikia tamati Agosti 23, mwaka huu jijini Nairobi, katika mashindano ya Zone V, yaliyofanyika Juni mwaka huu nchini Uganda alifanikiwa kuipeperusha vema bendera ya Tanzania katika kinyang’anyiro hicho dhidi ya wapinzani.

Comments are closed.