The House of Favourite Newspapers

Staa wa PSG Kylian Mbappe Aweka Rekodi Ya Kipee Atupia Mabao Matano

0
Kylian Mbappe

STAA wa PSG, Kylian Mbappe juzi aliteuliwa kwa nahodha wa Paris Saint-Germain kwa mara ya kwanza kwenye mchezo Coupe de France kufanikiwa kuweka rekodi ya kufunga mabao matano peke yake.

Akiwa na kitambaa mkononi, Mbappe amekuwa mchezaji wa kwanza katika historia ya Paris Saint-Germain kufunga mabao matano katika mchezo mmoja huku miamba hao wa Ligue 1 wakipata ushindi mnono dhidi ya Pays de Cassel.

PSG walikutana na timu hiyo katika hatua ya 32 bora ya Kombe la Ufaransa Jumatatu usiku, huku mabao matano ya Mbappe yakichangia ushindi wa 7-0.

Nyota huyo wa Ufaransa alikuwa ametajwa kuwa nahodha kwa mara ya kwanza tangu alipowasili Parc des Princes. Alicheza vyema na kuipeleka PSG katika hatua ya 16 bora.

HOTUBA ya TUNDU LISSU, ATEMA CHECHE, AMTAJA HAYATI MAGUFULI, AFUNGUKA MAZITO…

Leave A Reply