Kartra

Staa Yanga: Nabi Anza na Carlinhos Weka Nje Fei Toto

MSHAMBULIAJI wa zamani wa Yanga, Makumbi Juma, amesema anatamani kumuona Kocha wa Yanga, Nasreddine Nabi akimpanga kiungo Carlos Carlinhos dhidi ya Simba pembeni ya Mukoko Tonombe na si Feisal Salum ‘Fei Toto’.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Makumbi Juma alisema: “Nimependa sana walivyocheza kwa pamoja Carlinhos na Mukoko katika mechi zilizopita, natamani katika mchezo dhidi ya Simba pia kocha wa Yanga awatumie, naamini ushindi utapatikana.

 

“Carlinhos anajua kupiga pasi fupifupi, ndefu na anatengeneza nafasi nyingi kwa uharaka zaidi tofauti na Feisal ambaye yupo taratibu katika kutengeneza mashambulizi ya timu, hivyo natamani mtu wa kucheza na Mukoko Tonombe pale kati awe Carlinhos badala ya Feisal.”

STORI: MARCO MZUMBE, Dar es Salaam


Toa comment