The House of Favourite Newspapers

Staili ya ‘pushapu’ ya Magufuli yashika kasi!

0

PUSH UP WASANII (3)Dustan Shekidele, Morogoro
Jambo limezua jambo! Staili ya kupiga ‘pushapu’ iliyoasisiwa na mgombea wa nafasi ya urais kwa ‘leseni’ ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Pombe Magufuli ‘JM’ alipokuwa akijinadi kwenye kampeni zake katika Viwanja vya Kayanga wilayani Karagwe, Kagera hivi karibuni inazidi kushika kasi kila kona ya nchi.

PUSH UP WASANII (2)
Wakiwa mkoani hapa wikiendi iliyopita kumnadi Dk. Magufuli, baadhi ya mastaa wakiongozwa na wale wa Bongo Movies waliohamia CCM kutoka Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Aunt Ezekiel Grayson na Vincent Kigosi ‘Ray’ walioko kwenye Kampeni ya Tumestuka ndiyo waliokuwa wakiongoza jahazi.

PUSH UP WASANII (1)Ishu hiyo ilijiri kwenye Viwanja vya Shule ya Msingi Kiwanja cha Ndege mkoani hapa ambapo Aunt na Ray waliitwa jukwaani na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye ndipo wakafanya zoezi hilo ambalo kwa sasa ndiyo habari ya mjini.

PUSH UP WASANII (4)Wengine waliowaunga mkono ni Juma Nature, Inspekta Haroun, Husna Sajenti, Kitale, Stan Bakora, Kupa na wengine kibao.

PUSH UP WASANII (5)
Akizungumza na wananchi, Aunt alisema: “Tumeshtuka, tumetoka kule kwa mzee wa nywele nyeupe na sasa tumetinga kwa tingatinga Magufuli ‘so’ hapa ni kazi tu.”

PUSH UP WASANII (2)Kwa upande wake Ray alifunguka: “Tumekuja CCM kumsapoti Magufuli.”
Mbali na mastaa hao, watu mbalimbali wamekuwa wakijirekodi na kupiga picha wakipiga pushapu kisha kutupia kwenye mitandao ya kijamii kuonesha kuwa wanamuunga mkono Magufuli anayeendelea na kampeni zake ambapo jana alimalizia Shinyanga na leo yupo mkoani Mbeya.

Leave A Reply