The House of Favourite Newspapers

Stamina, Young Killer Kukinukisha Mkesha Mwaka Mpya

Stamina.

MARAPA wakali Bongo, Stamina na Young Killer wanatarajia kuangusha shoo ya nguvu katika mkesha wa Mwaka Mpya kwenye Ukumbi wa Dar Live, Mbagala Zakhem jijini Dar.

Mbali na wakali hao, usiku huo wa Desemba 31 unatarajiwa kupambwa na wasanii wengine wakali wakiwemo Jay Mo, Coyo, Q Boy Msafi, Sholo Mwamba na Dullvan. Shoo hiyo inatarajiwa kuanza mishale ya saa 12 jioni hadi majogoo.

Young Killer.

Meneja wa Ukumbi wa Dar Live, Rajab Mteta ‘KP’, amesema, kama ilivyo kawaida ya Dar Live huwa hawakosei katika suala zima la kutoa burudani hivyo mashabiki wafike kwa wingi maana siku hiyo itakuwa ni zaidi ya burudani kwa kiingilio cha sh. 5000 tu.

“Tuna listi kubwa tu ya wasanii, wameahidi kufanya mambo ya tofauti ambayo hayajawahi kufanyika kabla. Uzuri pale Dar Live kuna kila kitu, mambo ya vyakula, vinywaji ndani ni vya kumwaga. Ulinzi ni wa nguvu hivyo mashabiki waje tu kuukaribisha mwaka kwa shoo yenye hadhi yao,” alisema KP.

KP alisema mbali na orodha hiyo kubwa ya wasanii, wanatarajia pia kuwa na special appearance (staa mualikwa) ya msanii wa Bongo Movies, Esha Buheti hivyo mashabiki wa muvi na wasio wa muvi wanaweza kupata nafasi nzuri ya kujiachia naye, kupiga naye picha za kumbukumbu.

DAR ES SALAAM

Stori: Mwandishi Wetu, Amani.

Comments are closed.