The House of Favourite Newspapers

Stanbic Yatoa Misaada Wodi ya Wajawazito Hospitali ya Mwananyamala

0

Katika hatua ya kuimarisha huduma za afya, hasa kwa akina mama na watoto wachanga, Benki ya Stanbic Tanzania imechangia vifaa vya matibabu muhimu kwa Hospitali ya Mwananyamala.

Msaada huu wenye thamani ya Tsh milioni 19 unatarajiwa kuongeza uwezo wa hospitali katika kutoa huduma bora zaidi za uzazi. Vifaa vilivyotolewa ni pamoja na kifaa cha kufuatilia wagonjwa (Patient Monitor), Vacuum extracors sita, Seti sita za upasuaji wa Kaisaria na Karatasi za Mackintosh, Karatasi hizi za matumizi moja zitasaidia kudumisha usafi katika mazingira ya upasuaji.

Makabidhiano haya yaliudhuriwa na viongozi mbalinmbali kutoka sekta ya afya na benki. Meneja wa huduma kwa wateja, Lilian Abdulmalik aliongoza tukio la makabidhano akbalo pia lilihudhuriwa na Mratibu wa huduma za VVU na UKIMWI jijini Dar es salaam, Bw. Ayoub Kibao ambae alimuwakilisha Mganga Mkuu jijini Dar es salaam, Bw Mohamed Mang’unda.

Wageni wengine walikua pamoja na Mkurugenzii wa Wateja Binafsi , Omari Mtiga na Head of Compliance Rose Otaigo, Daktari Bingwa wa magomjwa ya wanawake, Dr Luzango Maembe, Diwani wa kata ya Makumbusho, Bw. Mohamed Ally Mohamed.

Hospitali ya Mwananyamala inayozalisha takribani watoto 800 kwa mwezi, ilikuwa inakabiliwa na upungufu mkubwa wa vifaa hivi muhimu, jambo lililokuwa likisababisha changamoto katika kutoa huduma bora za uzazi.

Kwa mujibu wa hospitali, vifaa vipya hivi vitawasaidia kuhudumia idadi kubwa zaidi ya wanawake wajawazito na kupunguza vifo vya mama na mtoto.

Akizungumza katika hafla ya makabidhiano, Mkurugenzi wa Benki Binafsi na ya Watu Binafsi katika Benki ya Stanbic, Omari Mtiga, alisisitiza umuhimu wa kuunga mkono jamii. Alisema kuwa “mbali na msaada huu, benki pia inashiriki katika miradi mingine ya maendeleo ya jamii kama vile upandaji miti kwa utunzaji wa Mazingira, ambapo wamefanikiwa kuoanda miti 50000 katika mikoa 12 katika mpamgo wa ‘Twende Butiama’ kwa ushirikiano na Vodacom Tanzania.

Mratibu wa Huduma za VVU na UKIMWI, Bw Ayoub Kibao, akipokea msaada huo kwa niaba ya Hospitali ya Mwananyamala alitoa shukrani za dhati kwa Benki ya Stanbic kwa msaada huo na akaomba wadau wengine kuiga mfano huo. Alisema kuwa “vifaa hivyo vitaboresha sana ubora wa huduma za afya kwa wanawake wajawazito na watoto wachanga. ZTUnahimiza wadau wengine wajitokeze kutoa kusaidia hata katika hospitali zingine ili kuweza kuokoa maisha.”

Msaada huu wa Benki ya Stanbic, ni hatua muhimu katika kuboresha afya ya mama na mtoto katika Hospitali ya Mwananyamala. Benki ya Stanbic imeonyesha umuhimu wa ushirikiano kati ya serikali, sekta binafsi, na jamii katika kuhakikisha kuwa kila mtu anapata huduma za afya bora.

Leave A Reply