The House of Favourite Newspapers

Staric amvutisha shisha demu wa Manyika

0

Stori:  Andrew Carlos

Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva, Richard Sitta ‘Staric’ ameshangaza watu baada ya kuvuja kwa picha zikimuonesha akila bata na demu anayefahamika kwa jina la Naima ambaye anatoka na kipa wa Simba, Manyika Jr.
Katika picha hizo, kuna ambazo zinamuonesha Staric akimpa Naima aina ya kilevi kiitwacho shisha, ambapo bila woga mrembo huyo anaivuta tena kwa ustadi mkubwa.

Baada ya kuzinasa picha hizo, paparazi wetu alimvutia waya Staric na kumbana kama ameamua kujiweka kwa mrembo huyo au kuna projekti inaendelea, akasema:
“Kama ni picha ambazo nimevaa suti nyekundu, hiyo ilikuwa kwenye kushuti video ya wimbo wangu uitwao Nipe Wakasema, siyo mtu wangu ana mpenzi wake.”

Leave A Reply