The House of Favourite Newspapers

Stars inaweza kufuzu Afcon mbele ya Uganda

Wachezaji wa timu ya Taifa Stars wakifanya mazoezi Uwanja wa Boko Jijini Dar.

 

TIMU ya soka ya Tanzania, Taifa Stars, Jumapili hii inatarajiwa kujitupa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kuvaana na Uganda ‘The Cranes’ katika mchezo wa kufuzu Kundi L.

 

Mchezo huo ni muhimu kwa Stars kupata ushindi yake ndani ya uwanja huku wakifuata maelekezo ya kocha mkuu wa timu hiyo ambaye ni Mnigeria, Emmanuel Amunike.

Wakati tukiwapa matumaini ya ushindi wachezaji wetu, bado sapoti kubwa ya mashabiki uwanjani inahitajika kipindi ili ijiweke katika nafasi ya kufuzu Fainali za Afrika (Afcon) zitakazofanyika nchini Misri, mwaka huu.

 

Championi Jumatano, linaamini kuwa hilo linawezekana kwa Stars kufuzu kama kila mchezaji atatimiza vizuri majukumu ambacho Taifa Stars itakuwa inapambana na Uganda, lengo likiwa ni kuwapa morali ya kujituma zaidi ili wavune matokeo chanya.

Championi Jumatano, linaamini mchezo huo siyo mwepesi kutokana na ubora wa kila timu kwa maana ya Taifa Stars ambao ndiyo wenyeji, lakini pia wapinzani Uganda.

 

Uganda inaongoza katika kundi lao wakiwa na pointi 13, wakifuatiwa na Lesotho 5, Tanzania 5 na Carpe Verde 4. Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Taifa Stars

 

PICHA: MUSA MATEJA | GPL

Comments are closed.