The House of Favourite Newspapers

Stars kujipima ubavu kwa Waarabu wa Misri

KUELEKEA michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) ambayo itafanyika Juni 21 hadi Julai 19, mwaka huu nchini Misri, timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars inatarajia kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Misri kwenye Uwanja wa Bourg Al Arab, Juni 13, mwaka huu.

 

Stars ambao walifuzu baada ya kuifunga Uganda mabao 3-0 wanatarajia kufungua pazia lao kwa kucheza na timu ya Algeria katika Afcon.

 

Akizungumza na Championi Ijumaa, Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Clifford Ndimbo alisema mchezo huo utakuwa wa kujipima nguvu kuelekea michuano hiyo na kukiweka sawa kikosi cha Taifa Stars.

“Taifa Stars wanatarajia kucheza na Misri katika mchezo wa kirafiki utakaopigwa kabla ya michuano hiyo kuanza ambapo ni kwa ajili ya kujiweka sawa na michuano ya Afcon,” alisema Ndimbo

Stori na Ibrahim Mressy

Comments are closed.