The House of Favourite Newspapers

Stars yaanza kazi, Kili Stars hiyo Chalenji cup

0

WAKATI Taifa Stars ikianza mazoezi jana jioni kujiandaa na mechi ya kufuzu Kombe la Dunia 2018 dhidi ya Malawi, Tanzania Bara imethibitisha kushiriki Kombe la Chalenji mwaka huu.

Jana jioni kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, kikosi cha Taifa Stars kilifanya mazoezi chini ya Kocha Charles Mkwasa tayari kwa mchezo na Malawi Oktoba 7, mwaka huu uwanjani hapo.

Wakati huohuo, timu ya Taifa ya Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars’ imethibitisha kushiriki michuano ya Kombe la Chalenji itakayofanyika Ethiopia kuanzia Novemba 21 hadi Disemba 6, mwaka huu.

Kilimanjaro Stars imeungana na nchi nyingine 12 wanachama wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) kushiriki michuano hiyo mikubwa Afrika Mashariki na Kati.

Nchi wanachama wa CECAFA ni Tanzania Bara, Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda, Ethiopia, Eritrea, Djibouti, Somali, Sudan, Sudan Kusini na Zanzibar.

Leave A Reply