The House of Favourite Newspapers

Stars Yaanza Safari ya Kuitafuta AFCON

0

KIKOSI cha timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars tayari kimeanza kambi ya kujiandaa na michezo ya kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) dhidi ya Equatorial Guinea na Libya.

 

Kikosi hicho ambacho kiko chini ya Mdenmark, Kim Poulsen kilianza kambi hiyo juzi Jumatatu, ambapo kuelekea michezo hiyo, Stars inatarajia kuwa na michezo miwili ya kirafiki dhidi ya Kenya.

 

Februari 26, mwaka huu Kocha Mkuu wa Stars, Poulsen alitangaza kikosi cha wachezaji 40 kwa ajili ya michezo hiyo ambapo watacheza mchezo wa kwanza dhidi ya Kenya Machi 15, na kurudiana Machi 18.

Stars itacheza na Equatorial Guinea Machi 25, huku ule wa Libya ukitarajiwa kupigwa Machi 28, au 30 kuendana na ratiba ya Shirikisho Afrika (Caf).

 

Akizungumza na Championi Jumatano, meneja wa kikosi cha Stars, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ alisema nyota wengi ambao tayari wamemaliza majukumu yao ya klabu wameripoti kambini.

 

“Kikosi cha Taifa Stars tayari kimeanza maandalizi kuelekea michezo yetu ya kirafiki dhidi ya Kenya, na ile ya kutafuta tiketi ya kufuzu kushiriki michuano ya AFCON dhidi ya Equatorial Guinea na Libya.“

 

Sehemu kubwa ya wachezaji ambao waliitwa tayari wamesharipoti kambini, na kwa wale walio na ruhusa maalum ya kumaliza majikumu yao ya klabu tunatarajia kuendelea kuwapokea kulingana na ruhusa zao.

Leave A Reply