stars yafuzu AFCON 2025
Timu ya taifa ya Tanzania Taifa stars, imefanikiwa kufuzu kucheza michuano ya kombe la mataifa ya Afrika AFCON itakayofanyika nchini Morroco mwakani, baada ya kuifunga Guinea bao 1-0 na kufikisha alama 10.
Msuva ameiandikia stars bao pekee baada ya pasi safi ya Mudathiri Yahya Abbas, na kuifanya Tanzania kujiongezea alama tatu na na kupanda mpaka nafasi ya pili wakiwashusha Guinea nafasi ya tatu Kwa tofauti ya alama moja
Tanzania inaungana na vinara wa kundi H DR Congo, wenye alama 12 ambao baadaye majira ya saa Moja watakabiliana na Ethiopia katika mchezo wa mwisho huku Ethiopia wakiwa wanaburuza mkia na alama moja.
Hii ni mara ya nne kwa Tanzania kushiriki michuano ya kombe la mataifa AFCON huku katika awamu mbili za mwisho mwaka 2019 ( misri) na mwaka 2023 (Ivory coast) waliishia hatua ya makundi.
Msuva baada ya kufunga hii leo amefikisha idadi ya mabao 24 nyuma ya Mwisho Ngassa mwenye mabao 25, wakiwa ni watanzania wenye mabao mengi zaidi katika timu ya Taifa.