Stars Yapoteza Dhidi ya Benin kwa Mkapa

TIMU ya Tanzania Taifa Stars leo Oktoba 7, 2021 imekubali kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Benin kwenye mchezo wa kufuzu fainali za kombe la dunia.

 

Stars ilipoteza nafasi za wazi za kufunga kwenye kipindi cha kwanza ambazo zingetumiwa vema huenda zingebadili matokeo.

Bao pekee la Benin limefungwa na mshambuliaji Steve Mounie dakika ya 72 ya mchezo, baada ya ushindi huu Benin wanaongoza msimamo wa kundi J kwa kufikisha alama 7, wakifuatiwa na DRC yenye alama 5 baada ya ushindi dhidi ya Madagascar.

 

Kikosi cha Stars kitaondoka nchini  kesho kuelekea Benin na Ockota 10, stars itakuwa na kibarua kigumu dhidi ya Benin.706
SWALI LA LEO

Kupanda Kwa Bei ya Mafuta Nchini, Nini Kifanyike Kupunguza Bei?
Toa comment