The House of Favourite Newspapers

Stars yatoka sare ya bao 2-2 na Algeria Taifa

0

Maguli 1Wachezaji wa Timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ wakishangilia moja ya bao.

Maguli 4

Mashabiki wakishangilia.

Mbwana Samatta akishangilia goli lake alilofunga dhidi ya Algeria

Mbwana Samatta akishangilia goli lake alilofunga dhidi ya Algeria.

Timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ imeeshindwa kuchomoza  na ushindi baada ya kulazimishwa sare ya kufungana magoli 2-2 dhidi ya timu ya taifa ya Algeria kwenye mchezo wa kwanza wa kuwania nafasi ya kupangwa kwenye makundi kwa ajili ya kuwania kufuzu kushiriki michuano ya kombe la dunia itakayofanyika mwaka 2018 nchini Urusi leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Elius Maguli alianza kuifungia Stars bao la kuongoza dakika ya 43 kipindi cha kwanza akiunganisha kwa kichwa krosi ya mlinzi wa kushoto Hajji Mwinyi. Goli hilo likaipeleka Stars mapumziko ikiwa mbele kwa bao 1-0.

Algeria walisawazisha goli dakika chache baada ya kipindi cha pili kuanza mfungaji akiwa ni Slimani Islam bao ambalo limefungwa kutokana na uzembe wa walinzi wa Stars.

Dakika za mwanzo za kipindi cha pili Stara ilicheza mpira wa kasi na kufanikiwa kupata goli la pili dakika ya 54 lililofungwa na Mbwana Samatta baada ya kuichambua safu ya ulinzi ya Algeria kisha kufunga goli kwa ustadi wa hali ya juu.

Muda mfupi baada ya Stars kupata goli la pili kocha alifanya mabadiliko kwa kumpumzisha Elius Maguli na nafasi yake kuchukuliwa na Mrisho Ngassa wakati Said Ndemla aliingia kuchukua nafasi ya Muthir Yahya.

Dakika ya 71 kipindi cha pili, Slimani Islam alifunga goli la kwanza kabla ya kuisawazishia Aligeria dakika ya 74 goli lililotokana na kutoelewana kwa safu ya ulinzi ya Stars na kutoa mwanya kwa Slimani kuisawazishia timu yake.

Kikosi cha Stars: Ally Mustafa, Shomari Kapombe, Haji Mwinyi, Nadir Haroub, Kelvin Yondani, Himid Mao, Thomas Ulimwengu, Mudathir Yahya, Mbwana Samatta, Elius Maguli na Farid Musa.

Wlioanzia kwenye benchi: Ailishi Manula (GK) Salim Mbonde, Mohamed Hussein, Simon Msuva, John Bocco, Mrisho Ngassa na Malimi Busungu.

Leave A Reply