The House of Favourite Newspapers
gunners X

StarTimes Kuonyesha Kombe la FA Uingereza

0
Meneja Masoko wa kampuni ya Star Media, David Malisa, akimkabidhi jezi mwandishi wa michezo, Sada Akida, wakati wa uzinduzi wa StarTimes kuanza kuonyesha michuano ya Kombe la FA Uingereza, jijini Dar es Salaam leo.  Katikati (mwenye jezi ya Chelsea) ni Mhariri Mtendaji wa magazeti la Global Publishers, Saleh Ally.

KAMPUNI ya Star Media kupitia brand yake ya StarTimes, imepata kibali cha kuonyesha michuano ya Kombe la FA (Emirates FA Cup) ikianza na ufunguzi wake kwa mchezo wa Ngao ya Jamii (FA Community Shield) ambapo watakuwa wakirusha matangazo ya mechi zote mubashara kutoka nchini Uingereza.

 

Akitoa ufafanuzi wa kibali hicho,  Meneja Masoko wa kampuni hiyo, David Malisa, amesema, StarTimes imepata rasmi kibali hicho ambacho kitakuwa ni mahususi kwa kurusha michezo hiyo katika nchi zote za kusini mwa jangwa la Sahara kupitia lugha mbalimbali,  kibali ambacho kitadumu mpaka mwishoni mwa mwaka 2021.

Saleh Ally akimkabidhi jezi mmoja wa waandishi wa habari za michezo.

“Kwa niaba ya Mkurugezi wetu wa Idara ya Michezo kutoka makao makuu yaliyopo Beijing, China, Shi Maochu, ametuambia kuwa hii ni hatua kubwa kwa michuano ya Emirates FA na Emirates Community Shield kurushwa kwetu kwa sababu yanajumuisha timu zote kubwa na bora zilizopo nchini Uingereza, hivyo tuna furaha kubwa sana kuwa sehemu ya kuonyesha michuano hiyo.

“Tunatambua wazi kuwa Watanzania wengi ni wapenzi wa mpira wa miguu, hivyo kwa kutambua hilo na ndiyo maana nasi tumezingatia hili kwa kuwasogezea matangazo yetu karibu ambapo watapata burudani ikiwa ni sambamba na michuano ya kimataifa ya Coppa Italia, na Bundesliga lakini pia baadhi ya ligi za Ulaya kama UEFA Europa League na Euro 2020.


Malisa aliongeza kwa kusema: “Pamoja na uwepo wa michuano mingi na mikubwa kama hiyo, tutaendelea kuwaletea maudhui mbalimbali kwa gharama nafuu kabisa hususani ndani ya mwaka huu wa 2020 ili tuweze kukidhi matarajio ya watazamaji wetu kwani mashindano haya ya Kombe la Emirates FA 2019/2020 yataanza kurushwa rasmi Januari 4 mwaka huu kwa maana ya kesho Jumamosi kupitia king’amuzi pendwa cha StarTimes.

Mtangazaji wa habari za michezo, Shaffih Dauda (wa pili kushoto), akimkabidhi jezi mshindi aliyeuliza  maswali katika hafla hiyo, ambaye ni mwandishi wa Global Publishers, Musa Mateja

“Lakini lazima watazamaji wetu wakumbuke kwamba matangazo haya yatakuwa mubashara kupitia chaneli nane za michezo zilizopo kwenye king’amuzi chetu ila pia tutarusha kupitia APP yetu ya StarTimes, hivyo unatakiwa kulipia mapema king’amuzi chako kupitia bando la Uhuru kwa shilingi 18,000 tu hili kwa watumiaji wa antenna na shilingi 21,000 kwa watumiaji wa dish,” amesema Malisa.

Leave A Reply