The House of Favourite Newspapers

Stella Joel: hili ni pigo kubwa kwangu

0

stella joel

KAatibu Mwenezi wa Chama cha Muziki wa Injili Tanzania, Stella Joel

Na Gladness Mallya

KATIBU Mwenezi wa Chama cha Muziki wa Injili Tanzania, Stella Joel amesema kifo cha mumewe Yeronimo Mwalo ni pigo kubwa kwake linalohitaji maombi ya kila siku.

Akizungumza kwa huzuni, Stella alisema mumewe alifikwa na umauti Ijumaa iliyopita katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ambako alilazwa kwa muda wa siku nne akisumbuliwa na uti wa mgongo.

“Kweli nimepigwa jamani, nahitaji tu maombi maana peke yangu siwezi, nilikuwa nimemzoea mume wangu, nilimpenda lakini Mungu amempenda zaidi, ukweli naumia,” alisema Stella.

Mwili wa marehemu Mwalo uliagwa Jumatatu katika Kanisa la Pentekoste Light House lililopo Ubungo, Dar na kusafirishwa kwenda katika Kijiji cha Mbiwili, Iringa na kuzikwa jana Jumanne.

Leave A Reply