Stephen Sey Atimkia Misri

KWA mujibu wa mwandishi nguli wa michezo barani Afrika Nuhu Adams, mshambuliaji wa Namungo Fc, Steven Sey inaripotiwa amejiunga na  El Sharkia El Dokhan FC inayoshiriki ligi kuu ya Misri.

 

Sey mbaye ni raia wa Ghana alifunga mabao 5, katika mechi 11 alizocheza  kwenye  kombe la shirikisho Afrika na kuisadia kutinga hatua ya makundi ya michuano hiyo.

 

Straika huyo mwenye umri wa miaka 27 alijiunga na Namungo msimu uliopita akitokea Singida United ambayo ilishuka daraja,  na kufanikiwa kuipa makali safu ya ushambuliaji ya timu hiyo mpaka sasa bado Namungo Fc hawajazungumzia kuhusu dili hilo.

 


Toa comment