The House of Favourite Newspapers

Stesheni za Treni Uingereza Zapigwa na Shambulio la Kimtandao

0

Stesheni 19 za reli nchini Uingereza, zikiwemo 10 katika Jiji la London, zimepata athari baada ya kupigwa na shambulio kubwa la mtandao linaloathiri mifumo ya Wi-Fi ya umma kwa abiria.

Shirika la Network Rail limethibitisha kuwa vituo vya London Euston, Manchester Piccadilly, Liverpool Lime Street, Birmingham New Street, na Glasgow Central ni miongoni mwa vilivyoathirika.

Jeshi la Polisi Uingereza limeanzisha uchunguzi baada ya wasafiri waliokuwa wakiingia kwenye Wi-Fi katika vituo hivyo kuripoti kuona ujumbe unaotishia kutokea kwa mashambulizi ya kigaidi barani Ulaya.

Mifumo ya Wi-Fi katika vituo vilivyoathirika inasimamiwa na Kampuni ya Telent ambayo pia inasimamia Wi-Fi za mashirika mengine.

Shambulio hilo limefanya ukurasa wa kuingia wa Wi-Fi kusomeka We Love ou, Europe kisha kufuatiwa na vitisho kuhusu mashambulizi hayo ya kigaidi, jambo lililozusha taharuki kubwa kwa abiria.

Leave A Reply