STEVE AJIGAMBA KULINDWA NA JB

Steven Mengere ‘Steve Nyerere’

MUIGIZAJI kutoka Bongo Movie, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ usiku wa kuamkia Jumatatu alizua gumzo baada ya kujigamba ukumbini kuwa bodigadi wake wa sasa ni Jacob Steven ‘JB’.  

 

Tukio hilo lilijiri katika Hoteli ya Hyatt Regency, Posta jijini Dar kulipokuwa na hafla ya kuzindua taasisi ya kusaidia watu wenye ulemavu wa ngozi pamoja na bidhaa ya manukato ya De La Boss iliyoandaliwa na Ofisa Habari wa Klabu ya Simba, Haji Manara.

 

Katikati ya hafla hiyo, Steve aliyekuwa ameongozana na JB alijigamba mbele ya watu kuwa kwa sasa analindwa naye jambo liliolofanya wengi kuangua vicheko. “Nina bodigadi huyu hapa (JB) na mimi nimekuwa mmojawapo kati ya wanaolindwa,” alisikika Steve.

 

Baada ya kuisha kwa shughuli hiyo, wawili hao waliongozana kutoka nje na walipofika ndipo kimbembe kikaanza baada ya Steve kumuamrisha JB akamsogezee gari lake. Hata hivyo, JB hakukubaliana naye na kila mmoja kufuata usafiri wake.

Stori: Musa Mateja.

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

Loading...

Toa comment