The House of Favourite Newspapers

Steve Amfungukia T.I.D Katika Bifu la Mastaa

Steven Mengere ‘Steve Nyerere’

SEKESEKE la madawa ya kulevya limeendelea kuibua mengi ambapo muigizaji na mchekeshaji mahiri nchini, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ amemfungukia msanii wa Bongo Fleva, Khalid Mohammed ‘T.I.D’ akidai msanii huyu wakati wake umepita na sasa ni wakati wake (Steve),  hivyo lazima awe na heshima.

Steve amefunguka hayo katika kipindi cha Enewz cha EATV   kilichorushwa jana.

Steve Nyerere na msanii mwenzake wa Bongo Movi

Katika mwendelezo wa kurushiana maneno,  awali T.I.D alishawahi kufunguka na kudai Steve alizusha kuwa yeye kapewa pesa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

“Siwezi kubishana  na T.I.D mtu ambaye akiona gari analikimbilia apate chochote kitu, kwa hiyo nikibishana naye ni kama napoteza muda, halafu mimi na TID ni kama vidole,  kuna kikubwa na kidogo.  Yeye wakati wake ulishapita,  huu ni wakati wa Steve lazima ajenge heshima, ” alisema Steve

Salum Milongo/GPL

Comments are closed.