The House of Favourite Newspapers

Steve Job akumbukwa baada ya kifo chake miaka minne iliyopita

0

MWASISI mwenza wa kampuni la zana za kompyuta la Apple, Steve Jobs, amekumbukwa leo na kampuni lake na walimwengu baada ya kufariki miaka minne iliyopita.

Mwasisi mwenza wa kampuni la zana za Kompyuta la Apple, Steve Jobs.

Kiongozi wa kampuni hilo, Tim Cook, na viongozi wengine wa kampuni hilo waliadhimisha tukio hilo kwa kummwagia sifa mwenzao huyo aliyefariki na kuliachia sifa kubwa kampuni hilo maarufu duniani.

Katika barua-pepe aliyoituma kwa wafanyakazi wa Apple, Cook alimkumbuka Jobs kama mwanafamilia wao na kwamba alikuwa chanzo cha nguvu ya ufanisi wa kampuni hilo na bidhaa zake zinazokubalika duniani kote.

“Jobs aliipenda familia yake, aliwapenda wafanyakazi wa Apple na watu wengine aliofanya nao kazi kwa karibu,” aliandika Cook katika barua-pepe hiyo.

Ujumbe huo wa Cook ulikuwa miongoni mwa ujumbe lukuki uliotumwa na walimwengu kwenye tovuti ya Apple. Kumbukumbu hiyo itakwenda sambamba na kuzinduliwa kwa filamu iitwayo ‘Steve Jobs’.
 IMac.

Hata hivyo, mjane wa Jobs aitwaye, Laurene Powell Jobs, amesemekana kutokubaliana na kuzinduliwa kwa filamu hiyo na kulitaka kampuni lililotayarisha filamu liitwalo Sony Pictures and Universal Pictures, kuachana na mpango huo.Filamu hiyo ambayo ina simulizi iliyoandikwa na Aaron Sorkin, inahusu maisha ya Jobs kutokana na simulizi za Walter Isaacson.

Moja ya bidhaa za Apple iPad Mini 4.

“Mama huyo amekataa kujadili chochote kuhusu simulizi hiyo ya Aaron licha ya watu kumbembeleza sana,” alisema prodyuza Scott Rudin akizungumza na jarida la Journal na kuongeza kwamba “alieleza alivyokuwa anakichukia kitabu hicho na kwamba filamu yoyote kuhusiana na kitabu hicho haiwezi kuwa sahihi.”

Jobs alifariki Oktoba 5, 2011, akiwa na umri wa miaka 56 kutokana na matatizo ya mfumo wa hewa uliozidisha matatizo ya ugonjwa wake wa kansa ya kongosho. Mtu huyo amebakia kuwa maarufu duniani kutokana na bidhaa za kampuni yake miongoni mwake zikiwa ni pamoja na zile za iMac na iPhone.

Leave A Reply