The House of Favourite Newspapers

Steve: Mtaniomba Msamaha Nikiwa Kwenye Jeneza!

0
Steven Mengere ‘Steve Nyerere’

Komediani mwenye jina kubwa Bongo, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ amewafungukia watu wake wa karibu akiwaambia kwamba, siku akifa hawataamini na huenda ikawa wameshachelewa kuyafanya ya muhimu juu yake.

 

Kwenye ukurasa wake wa Instagram, jana, Steve Nyerere alitupia maneno mazito kwenye posti huku akiweka picha za watu mbali mbali maarufu hapa Tanzania, akisema kuwa siku akifa watatamani kumuomba msamaha akiwa kwenye jeneza lake.

 

“Siku nikifa najua hata wanaonichukia hawataamini, wataniomba msamaha nikiwa kwenye jeneza, lakini itakuwa haina maana, wangine watasema, dah, tulimkosea sana na wangine watakuwa wamejifunza kitu kupitia mimi, siku nikifa…,” aliandika Steve Nyerere.

 

Baada ya Lissu Kuliamsha Dude, Serikali Yafunguka Sakata la Bombadier

Usipitwe na Matukio, Install ===>Global Publishers App

Sikiliza Hadithi za Mtunzi Eric Shigongo Hapa

Leave A Reply