The House of Favourite Newspapers

Nyerere Afunguka Wema Kuhamia CCM, Ataja Sababu za Kumjibu Polepole – (Video)

0
Steve Nyerere.

Muigizaji maarufu nchini, Steve Nyerere ambaye pia ni kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), amesema kuwa amefurahishwa sana na maamuzi ya msanii mwenzake, Wema Sepetu kurudi CCM akitokea katika Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) alikojiunga na mama yake tangu Februari mwaka huu.

 

Steve amesema kuwa maamuzi ya Wema hayajasababishwa na kesi yake inayomkabili ya madawa ya kulevya, wala hofu ya kuponea chupuchupu kubomolewa nyumba yao, badala yake ni mapenzi tu aliyokuwa nayo kwa CCM. Amesema ni hasira tu ndizo zilimuhamisha na kwa sasa zimekwisha ameamua kurudi nyumbani.

 

Aidha Steve Nyerere, ameongeza kuwa ujumbe wa Katibu Mwenezi wa CCM, Humphrey Polepole kumtaka Wema aendelee kubaki Chadema, hakupendezwa nao ila anachokiona ni kuwa alikuwa ameghafilikiwa tu na haikuwa kusudio lake, kwa maana wanachama wote waliowahi kukihama chama hicho na kurejea hawakuwahi kuwekewa vikwazo vya aina yoyote, hivyo kwa upande wa Wema atarudi vizuri kabisa.

VIDEO: MSIKIE STEVE NYERERE AKIFUNGUKA

Leave A Reply