The House of Favourite Newspapers

Steve Nyerere Alia na Majungu

KOMEDIANI maarufu Bongo, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ amelia na majungu kuwa, kama wasanii wa Bongo Movies wangeya-punguza, basi wangesonga mbele.

Steve aliliambia Ijumaa Wikienda kuwa, kama wasanii wengi wangekuwa makini katika vitu vya maendeleo na kuyaepuka majungu wangeendelea.

“Unajua Bongo Movies wangependa maendeleo zaidi kuliko majungu, wangefika mbali sana, lakini kwa vile hawataki kubadilika watabaki hivyohivyo,” alisema Steve ambaye hivi karibuni alidai kuzushiwa kuwa na ngoma.

Stori: Imelda Mtema, Dar

Comments are closed.