The House of Favourite Newspapers

STEVE NYERERE AMLIPUA MAMA KANUMBA, AFUTA NAMBA ZAKE

MKALI wa Bongo Movies ambaye pia ni kiongozi wa wasanii wa filamu nchini, Steven Mengele ‘Steve Nyerere’ amevunja ukimya na kumlipua Mama Kanumba, Flora Mtegoa aliyedai hajaridhishwa na kubadilishiwa adhabu kwa msanii Elizabeth Michael ‘Lulu’ ambaye Novemba 13, 2017 alihukumiwa kifungo cha miaka miwili jela kwa kosa la kumuua Kanumba bila kukusudia.
Steve amesema kwamba ameamua kufuta namba ya Mama Kanumba kwa sababu hana shughuli naye wala asitake kushindana na maamuzi ya serikali kwani hata yeye ilimsaidia alipohitaji msaada.
“Nimekasirika sana kwa kauli za Mama kanumba, na namba yake nimeifuta kabisa, nimeona hana shughuli, kwa sababu anaongea vitu ambavyo havipo yaani, na sioni kama kina tija. Kuna mambo mengune siyo unakurupuka tu kuongea, unatakiwa ukae na watu wakupe ushauri.
“Yeye si mtu wa kugombana na serikali, alipokufa Kanumba srikali ilimsaidia sana huyu mama, hata nyumba aliyokuwa anaishi serikali ilimpa, hakutakiwa kujibu chochote, alitakiwa kunyamaza na maisha yakaendelea.
“Hata kama ungemfunga Lulu miaka 100, Kanumba atarudi? Usiilazimishe watu au jamii yako ikuone umeshindwa, wala usiilazimishe jamii ikuone una roho mbaya, hapaswi kulalamika sana kwa sababu hana uhakika kama kweli aliua, lakini pia wawili hao walikuwa kwenye mahusiano,” amesema Steve.

Comments are closed.