The House of Favourite Newspapers

Steve Nyerere Amvaa Mwijuaku Kisa Uspika

0

MSANII Maarufu wa vichekesho nchini, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ ameamua kuvunja ukimya na kuwalipua baadhi ya watu waliochukua fomu kuwania u-spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akidai kuwa baadhi yao hawana sifa za kukalia kiti hicho.

 

Steve amesema hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram ikiwa ni saa baada ya Mtangazaji wa CloudsFM kipindi cha LEO TENA na kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Burton Mwemba maarufu kwa jina la Mwijaku kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya U-spika leo  Ijumaa Januari 14, 2022.

 

“Nimekaa naongea Mwenyewe Mpaka Mwijaku Kachukua Fomu, Si mbaya ila kuna haja ya marekebisho kipengele cha Spika, vigezo na Masharti Maana Tunaenda kuchagua MTU ambaye kisheria ni muhimiri wa Bunge , Na kikatiba ni Muhimiri wa 3. Sasa kila nikitazama Wagombea wanao Miminika najiuliza ni Fashion Au…?”

 

Zoezi la kuchukua fomu hizo kuomba nafasi ya kuwania kiti cha Uspika katika Ofisi za CCM Lumumba jijini Dar es Salaam, linaloendelea ili kuanza kwa mchakato wa kumpata mrithi wa Job Ndugai ambaye alijiuzulu wadhifa huo.

Leave A Reply