Steve Nyerere: Bora Alikiba!

MSANII maarufu wa Bongo Movie, Steve Nyerere,  amempongeza msanii wa Bongo Fleva, Alikiba, baada ya kuwaombea bajeti wasanii wa Bongo Movies, kwa Rais John Magufuli ya kutengenezwa documentary ya maisha ya Baba wa Taifa Mwl. Julius  Nyerere ambayo itaelezea maisha yake.

 

Amempongeza Kiba na na kusema hiyo ndiyo maana msanii huyo anaitwa King wa muziki wa Bongo Fleva (Mfalme wa Bongo Fleva).

 

Ameongeza kuwa watu wengine walikuwa wanaipuuza sana Bongo Movie lakini Kiba ameonyesha kuwa tasnia hiyo ina umuhimu mkubwa. Pia amewaponda wale wanaosema wasanii wengi wanakipigia kampeni CCM kwa kuwa njaa zinawasumbua.

Toa comment