The House of Favourite Newspapers

Steve Nyerere Majanga Tena

0

NA GLADNESS MALLYA | GAZETI LA AMANI | DAR ES SALAAM

Baada ya hivi karibuni nyumba yake kuvamiwa na kunyofolewa madirisha, msanii wa vichekesho Bongo, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ amepata majanga tena kufuatia mwanaye kupotea katika mazingira ya kutatanisha.

Chanzo kilieleza kuwa motto huyo alitoweka nyumbani kwao, Kinondoni Mkwajuni, Dar siku tatu zilizopita na kumsababisha Steve kuwa na wasiwasi mkubwa kwamba huenda ametekwa au la kwani amejaribu kutafuta kila sehemu bila mafanikio.

“Yaani mwaka huu Steve ana majanga makubwa maana hata hajapumzika na tukio la kuibiwa, limetokea tena hili la kupotelewa na mwanaye ambaye ni mwanafunzi yaani ana haha kweli,” kilisema chanzo.

 

Baada ya kupata habari hizo, Amani lilimtafuta Steve ambaye alikiri kupotelewa na mwanaye anayejulikana kwa jina la Linda Raymond (17) ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha nne kwenye shule moja iliyopo wilayani Moshi, mkoani Kilimanjaro.

“Siku ya tukio ambayo ni Jumapili saa kumi na mbili jioni mwanangu alitoweka nyumbani kwangu Kinondoni Mkwajuni na nimejaribu kumtafuta kila kona lakini sijafanikiwa ambapo tulienda polisi na kufungua kesi kwa jalada OB/RB/697110/17.

“Nawaomba Watanzania wanisaidie jamani popote watakapomuona watoe taarifa kituo chochote cha polisi kwani ni mwanafunzi wa kidato cha nne halafu nimejaribu kwenda kuangalia kwenye mtandao wa simu mtu wa mwisho kuwasiliana naye inaonekana ni mwanaume amemtorosha, hatujui ni kwa lengo gani maana sasa hivi hofu kubwa isiwe ametekwa,” alisema Steve.

LIVE: Steve Nyerere Ataja Sababu za Kugomea Maandamano ya Bongo Movies

Leave A Reply