The House of Favourite Newspapers
gunners X

Steve: Sing’atuki Hata Kwa Dawa

0


Steve Nyerere au Tive Ake kama Wema anavypenda kumuita; ni komediani fundi wa michongo kunako Bongo Movies ambaye sakata lake la uteuzi wa kuwa Msemaji wa Shirikisho la Muziki Tanzania bado linazidi kukolea zaidi huku wasanii wakigawanyika pakubwa na kuahidi kulipatia uvumbuzi leo Jumatatu Machi 21, 2022.

Wapo wale wanaoona kwamba uteuzi wake kuwa msemaji na bwana mipango wa shirikisho ni haki na upande wa pili kuna wale wanaosema hakufaa kupewa nafasi kama hiyo kwa sababu yeye si msanii wa muziki.

Baada ya joto la shinikizo kupanda, hatimaye msemaji mteule, Steve amevunja ukimya wake na kutoa tamko lake kuhusu ishu.

Steve anasisitiza kwamba ameshateuliwa na kuchukua majukumu yake kama msemaji na mratibu wa mipango ya shughuli za muziki na katu hawezi kung’atuka hata kwa dawa.

“Nawaambia tu, sijiuzulu na wala sitoki. Nina nia ya kuendeleza industry ya nchi hii,” Steve.
Alipoulizwa kuhusu uwezekano wa wasanii kumtengua katika kikao ambacho wamekiitisha leo, Steve anasema kuna taasisi za mahakama na suala hilo litakaa kisheria zaidi kama wasanii wataamua kwenda katika mkondo huo.
Cc; @sifaelpaul

Leave A Reply