The House of Favourite Newspapers

Stonebwoy aachia albamu mpya ya 5th Dimension akiwashirikisha Stormzy, Davido, Mereba, Shaggy na wengineo

0
Msanii Stwoneboy kutoka nchini Ghana

 

Msanii mahiri wa Afro- Dancehall kutoka nchini Ghana aliyesainiwa na lebo ya Def Jam Records, Stonebwoy ameachia albamu mpya ya 5th Dimension, ikiwa ni albamu yake ya tano tangu alipoanza muziki.

Stonebwoy ambaye anaimba mchanganyiko wa muziki wa Reggae, Dancehall na Afro- Dancehall, tayari ameachia ngoma kadhaa za utangulizi kutoka katika albamu hiyo, ikiwemo Life & Money aliomshirikisha Stormzy, More of You, Therapy na Far Away.

Mbali na Stormzy, mastaa wengine walioshirikishwa katika albamu hiyo ni pamoja na Shaggy, Mereba, Davido na mwanamama aliyeshinda kadhaa za Grammy, Angelique Kidjo ambaye ameshirikishwa katika wimbo wa Manodzi.

Stonebwoy ambaye alianza muziki mwaka 2012, tayari ameshafanya ziara za kuutangaza muziki wake kwenye maeneo mbalimbali duniani, huku akishirikiana na mastaa wakubwa wa kimataifa kama Keri Wilson, Sean Paul, Trey Songz, Burna Boy, Alpha Blondie na wengine wengi.

Muziki wake umemfanya apate tuzo kadhaa ikiwemo ya BET katika kipengele cha Best International Act: Africa, Artist of the Year katika Tuzo za Ghana Music Awards na tuzo mbili za Billboard ambapo pia hivi karibuni, ameweka rekodi ya kuwa msanii wa kwanza kutoka nchini Ghana kufikisha streams milioni 100 katika jukwaa la Audiomack.

Pia amewahi kushiriki kwenye matamasha makubwa duniani ikiwemo Rotom

Sunsplash Festival lililofanyika mwaka 2019 nchini Hispania, Afro Nation lililofanyika nchini Puerto Rico mwaka 2020, Yam Carnival lililofanyika nchini Uingereza mwaka 2021 na hivi karibuni alishiriki katika Tamashala FIFA Fan Festival wakati wa Kombe la Dunia nchini Qatar.

Unaweza kuisikiliza albamu hiyo kwa kubofya 5th Dimension.

Leave A Reply