The House of Favourite Newspapers

Straika Mpya Yanga Atoa Kauli ya Kibabe Malengo yake ni Kuhakikisha Anawapa Makombe

0
Lazarus Kambole.

 

MSHAMBULIAJI mpya wa Yanga, Mzambia, Lazarus Kambole, amefunguka kuwa moja ya malengo yake ni kuhakikisha anaipa Yanga makombe mengi pamoja na kufikia malengo ya michuano ya kimataifa msimu ujao.

 

Kambole amejiunga na Yanga kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini ambayo ameachana nayo baada ya mkataba wake kumalizika.

 

Mshambuliaji huyo ana rekodi ya kufunga hat trick ya haraka zaidi kwa kutumia dakika nne kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika katika msimu wa 2017/18 akiwa na Zesco ya Zambia.

 

Kambole amelimbia Championi Ijumaa kuwa moja ya malengo yake makubwa ya kutua Yanga ni kuona inafakiwa kushinda mataji mengi ya ndani pamoja na kufanya vizuri katika michuano ya kimataifa msimu ujao.

 

“Nafahamu kwamba Yanga ni timu kubwa ambayo ina mashabiki wengi ambao presha yao kubwa ni kwa timu kufanya vizuri katika michuano ambayo itakuwa inashiriki, wajibu wangu ni kuona napambana kufikia malengo.

 

“Unajua hakuna kitu kikubwa kama unakuwa ndani ya timu ambayo inataka kufanya mambo makubwa katika ligi ya ndani kwa kuhakikisha wanashinda makombe mengi ya ndani na kufanya vizuri kimataifa hivyo katika hali yoyote lazima nipambane kufikia malengo ya timu,” alisema Kambole.

Stori na Ibrahim Mussa

SHANGWE la MAYELE, MAKAMBO na MSOLLA BAADA ya KOMBE – “LEO NI BATA TU, MSIMU UJAO TUTAJUA TU”

Leave A Reply