The House of Favourite Newspapers

Straika Wa Mazembe Awatuliza Simba Ligi ya Mabingwa Afrika

0
Jean Baleke

MSHAMBULIAJI wa Simba, Jean Baleke ameibuka na kuwatuliza mashabiki wa timu hiyo kwa kuwaambia bado anaimani kubwa na timu hiyo kufikia malengo yake katika Ligi ya Mabingwa Afrika licha ya kupoteza michezo yao miwili ya awali.

Baleke ambaye amejiunga na Simba kwa mkataba wa mkopo wa mwaka mmoja akitokea TP Mazembe, ametoa kauli hiyo kufuatia Simba kupoteza michezo miwili ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo walifungwa na Horoya ya Guinea bao 1-0 kabla ya kufungwa tena na Raja Casablanca kwa mabao 3-0.

Akizungumza na Championi Jumatano, Baleke alisema kuwa: “Nadhani ni wakati wa kutuunga mkono kwa sababu bado tuna nafasi ya kufanya vizuri katika mechi zilizobakia, kila mchezaji amekuwa kwenye wakati mgumu juu ya matokeo ya mchezo uliopita ambao matarajio yetu yalikuwa ni kupata ushindi.

“Kitu kikubwa ni mashabiki kuendelea kutupa sapoti wakati wote ili kuweza kupata ushindi kwenye mchezo wetu ujao dhidi ya Vipers kwa sababu kila mchezaji matarajio ni kuona tunaweza kufikia hatua kubwa katika michuano hii ingawa tumekuwa na matokeo ya kushangaza kwenye mechi zetu mbili zilizopita.”

Stori na Ibrahim Mussa, Spoti Xtra

”GOLI 1 KOCHA ANATAKA KUPANDA JUKWAANI” – ALI KAMWE AMVAA KOCHA ROBERTINHO wa SIMBA...

Leave A Reply