Straika wa Zamani wa Yanga Amchana Makavu Mayele, Amshauri Asibweteke

Mshambuliaji wa zamani wa Yanga raia wa Kenya Boniface Ambani

MSHAMBULIAJI wa zamani wa klabu ya Yanga Boniface Ambani amemshauri mchezaji wa Yanga na straika tegemeo wa timu hiyo Fiston Mayele kutobweteka na kuongeza juhudi kwani idadi yake ya magoli hairidhishi ukilinganisha na enzi zake wakati akiwa katika klabu hiyo.

 

“Nadhani amefunga zaidi ya bao kumi saizi lakini tuko mzunguko wa ngapi saizi? wa pili kwahivyo kidogo average scoring yake iko chini, wakati mimi nacheza Yanga timu zilikuwa 12 pekeyake sasa zipo 18 kwahiyo yeye mwenyewe kama Straika lazima aangalie Statistics zake asifunge bao moja tu akafurahi.”

Mshambuliaji wa Yanga Fiston Mayele

Amedai pia kuwa enzi zile anacheza Yanga wachezaji wazawa walinufaika zaidi na ujio wa wachezaji wa kigeni kwani waliwapa vitu ambavyo wazawa hawakuwa navyo na wazawa kama kina Jerry Tegete, pamoja na Gaudence Mwaikimba.

 

Kwa upande mwingine Ambani amedai kama uongozi wa Yanga utaamua kumpa nafasi yoyote ile ndani ya klabu hiyo yupo tayari kurudi kwani alikuwa na wakati mzuri klabuni hapo.

 

4234
SWALI LA LEO
YANGA/SIMBA KIMATAIFA
Baada ya usajili wa nguvu, mechi za Siku ya Wananchi na Simba Day kisha mechi ya ufunguzi wa Ligi Kuu ya Ngao ya Hisani, je, ni timu gani unaamini itafanya vizuri kimataifa?Toa comment