The House of Favourite Newspapers

Suarez, Baby Wake Wavamiwa na Vibaka Wakiwa Penzini

0

KIUNGO wa zamani wa Arsenal na Barcelona, Denis Suarez juzikati alivamiwa na vibaka nyumbani kwake huku yeye akiwa amefanya mtoko wa kimapenzi na mpenzi wake mrembo, Nadia Aviles.

 

Nyota huyo, 25, ambaye alifeli Arsenal alikuwa amefanya mtoko na mpenzi wake Nadia kusherehekea Mwaka Mpya.

 

Wakati wao wakiwa bize kimahaba, huku nyuma vibaka walivunja dirisha na kuingia nyumbani kwao kwa lengo la kuiba.

 

Hata hivyo, baada ya kuvunja, inaelezwa vibaka hao hawakupata kitu cha thamani kwao kuiba, wakaondoka mikono mitupu.

 

Suarez ambaye sasa anaichezea Celta Vigo na Aviles, wamekuwa wapenzi kwa mwaka na nusu sasa.

 

Nadia alisherehekea mwaka mpya kwa kutuma picha akiwa anambusu Suarez na chini yake akaambatanisha maneno haya: “Naahidi kuendelea kukutunza na kutunza penzi letu daima.”

BARCELONA, Hispania

Leave A Reply